MAONESHO

Uzinduzi wa maonesho hayo ya saba ya biashara ya Zanzibar yaliyoanza tarehe 4/1/2021 hadi tarehe 15/1/2021, yalizinduliwa rasmi na Mh Samia Suluhu Hassan. Katika maonesho hayo, viongozi mbali mbali akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu Mh Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Kazi , Uchumi na Uwekezaji Mh Mudrik Ramadhan Soraga , walishiriki katika maonesho hayo.